
Emmanuel Macron atampokea Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mjini Paris Jumatatu, Novemba 17, kwa ziara inayolenga “kuthibitisha tena kujitolea kwa Ufaransa kwa Ukraine” na “kudumisha kasi ya kazi inayofanywa katika suala la dhamana za usalama” kwa Kyiv, kulingana na Ikulu ya Élysée.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ziara hii ya tisa ya Volodymyr Zelensky nchini Ufaransa tangu kuanza kwa vita vilivyoanzishwa na Urusi tangu mwaka 2022 “itawezesha kuthibitishwa tena kwa ahadi ya muda mrefu ya Ufaransa kwa Ukraine na kudumisha kasi ya kazi inayofanywa katika suala la dhamana za usalama” ndani ya mfumo wa “umoja wa nchi zilizo tayari” zinazounga mkono Kyiv, Ikulu ya Elysée imeongeza.
Pia ziara hii itawezesha “majadiliano kuhusu changamoto za ushirikiano wa pande mbili, hasa katika sekta za nishati, uchumi, na ulinzi”, Elysée imebainisha.
Hayo yanajiri wakati Urusi imetekeleza shambulio jipya kubwa usiku wa jana kuamkia leo Ijuma katika mji mkuu wa Ukraine Kyiv.
Shambulio hilo limesababisha vifo vya watu wanne na angalau 18 kujeruhiwa, idara ya huduma za dharura imeripoti.
Milipuko mikubwa ilisikika katikati mwa jiji, na mifumo ya ulinzi wa anga iliwashwa dhidi ya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani na makombora. Meya wa Kyiv Vitali Klitschko, ambaye amekuwa amewahimiza wakazi kujificha, amesema kwamba “vikosi vya ulinzi wa anga vinafanya kazi Kyiv,” akibainisha “shambulio kubwa la adui katika mji mkuu.”