Wizara hiyo imesema hii ni mara ya kwanza kwa utawala mpya wa Trump kutangaza kuiuzia nchi hiyo silaha.

Akizungumzia hatua hiyo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Lin Jian amesema Marekani kuiuzia Taiwan silaha ni ukiukwaji mkubwa wa kanuni ya China moja na taarifa ya pamoja ya Marekani na muungano wa Sino unaozijumuisha China, Japan, Korea, na Vietnam hasa ya Agosti 17.

”Inakiuka kwa kiasi kikubwa mamlaka ya China na maslahi ya usalama, inakiuka sana sheria ya kimataifa, na kutuma ishara mbaya kwa vikosi vya Taiwan vinavyotaka kujitenga. China inapinga vikali suala hili.

Marekani ni muuzaji mkuu wa silaha kwa Taiwan na kizuizi muhimu kwa uwezekano wa shambulizi la China, lakini matamshi ya Trump juu ya Taiwan yamezua shaka juu ya nia yake ya kutetea kisiwa hicho cha kidemokrasia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *