
Kiongozi wa zamani wa waasi nchini DRC, Roger Lumbala, ambaye kesi yake imengia siku ya tatu leo Ijumaa, ametangaza kwamba ameanza mgomo wa kula. Akishtakiwa kwa kushiriki katika uhalifu dhidi ya ubinadamu, mshtakiwa anaendelea kukataa kufika mahakamani. Jaji mkuu wa Mahakama ya Paris amesoma taarifa iliyoandikwa na raia huyo wa Kongo na kuiwasilisha mahakamani. Inabaki kuamuliwa ikiwa mahakama hii ya Ufaransa ina mamlaka ya kumshtaki kiongozi huyo wa zamani wa waasi.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kama anavyofanya kila siku, jaji mkuu wa Mahakama ya Paris, Marc Sommerer, amebainisha kutokuwepo kwa Roger Lumbala. Kikao kimeahirishwa: amerudi dakika chache baadaye na kutangaza kwamba afisa wa gereza amempa hati, ambayo ingewasilishwa katika mjadala kama Kiambatisho kimoja. Ndani yake, mshtakiwa anatangaza kwamba anaanza mgomo wa njaa na kiu. Karani amempa jaji mkuu taarifa hiyo, ambaye ameisoma kwa sauti: “Sitambui mamlaka ya Mahakama ya Paris. Kifungu cha 689-11 cha Kanuni ya Utaratibu wa Jinai hakijaheshimiwa.”
Jaji mkuu ameendelea kusoma: “ICC haijatoa hati yoyote inayothibitisha kwamba hainishtaki. Kwa kukosekana kwa ziara ya wataalamu nchini DRC, haijawezekana kuthibitisha kama mahakamakatika ngai ya kitaifa inanishtaki.” Na hatimaye: “Bila cheti cha utawala, siwezi kuhudhuria.”
Suala la mamlaka ya Mahakama bado halijatatuliwa
Vyama vya kiraia pia vimemwuliza jaji mkuu kama uhalali wa mamlaka ya ulimwengu unatambuliwa na mahakama hii. Jaji amejibu kwamba hili litaamuliwa baada ya kusikilizwa, Alhamisi ya wiki ijayo, kwa wachunguzi kutoka Ofisi Kuu ya Kupambana na Uhalifu Dhidi ya Ubinadamu walioshiriki katika uchunguzi wa awali.
Jaji mkuu amesema kwamba mazingira si nzuri kwa mshtakiwa, ambaye kwa sasa anashikiliwa katika chumba kidogo mahakamani. Mipango mbadala itafanywa ili kumruhusu kurudi gerezani baada ya kukataa kwake kufika mahakamni.
Roger Lumbala alikamatwa mnamo Desemba 2020, alifaniwa uchunguzi mnamo Januari 4, 2021, na kushtakiwa mnamo 2023. Anashtakiwa tangu Novemba 12, 2025, mbele ya Mahakama ya Paris, kwa kushiriki katika uhalifu dhidi ya ubinadamu na njama ya kutenda uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa vitendo vilivyofanywa mashariki mwa DRC, haswa mnamo mwaka 2002. Kwa sasa anashtakiwa chini ya kanuni ya mamlaka ya ulimwengu. Hii ni kesi ya kwanza nchini Ufaransa inayomhusisha raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kuanzia Novemba 12 hadi Desemba 19, 2025, jaji mkuu wa Mahakama ya Paris na manaibu waendesha mashtaka wawili wa kupambana na ugaidi watachunguza jukumu la kiongozi huyu wa zamani wa waasi wa RCD-N, anayetuhumiwa kushiriki katika Operesheni “Futa Ubao” pamoja na Naibu Waziri Mkuu wa sasa wa DRC na kiongozi wa zamani wa waasi Jean-Pierre Bemba, ambaye wakati huo alikuwa mkuu wa kundi la waasi la MLC. Operesheni hii iliyokubwa na mauaji ya halaiki, ubakaji, na vitendo vya mateso, hasa dhidi ya raia wa Batwa na Nande. Roger Lumbala hakuwahi kushtakiwa.
Zaidi ya miaka ishirini baada ya matukio hayo, kesi hii ya mfano inategemea ripoti na ushuhuda mbalimbali kutoka kwa waathiriwa huko Haut-Uélé na Ituri. Kwa vyama vya kiraia, inawakilisha hatua ya kihistoria mbele dhidi ya kutokujali; kwa upande wa utetezi, shambulio dhidi ya uhuru wa Kongo.