Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya WFP ya Tathmini ya Mtazamo wa Dunia wa mwaka 2026, ambayo imetolewa leo tarehe 18 mwezi Novemba 2025,  na kueleza kuwa idadi hiyo ni zaidi ya mara mbili ya walioripotiwa mnamo mwaka 2019.

Hata hivyo, kupungua kwa ufadhili wa kibinadamu kunailazimu WFP kuipa kipaumbele huduma kwa takribani watu milioni 110 pekee sawa na theluthi moja ya wote wanaohitaji msaada wa haraka

WFP inahitaji kiasi cha dola bilioni 13 kutekeleza mpango wake wa mwama 2026, lakini makadirio yanaonesha huenda ikapokea chini ya nusu ya kiasi hicho.

Mkate unasambazwa kwa familia zinazoishi kwenye mahema huko Deir al-Balah, Gaza.

© WFP/Maxime Le Lijour

Mkate unasambazwa kwa familia zinazoishi kwenye mahema huko Deir al-Balah, Gaza.

Migogoro na tabianchi vyachochea njaa

Mkurugenzi Mtendaji wa WFP, Cindy McCain, amesema dunia inashuhudia “njaa za wakati mmoja” katika maeneo kama Gaza na Sudan, akisisitiza kuwa hali hiyo “haiwezi kukubalika katika karne ya 21.”

Duniani kote, njaa inazidi kuota mizizi,” amesema. “WFP imeonesha mara nyingi kwamba hatua za mapema, zenye ubunifu na ufanisi zinaweza kuokoa maisha. Lakini tunahitaji kuungwa mkono zaidi ili kuendelea kuwafikia walio hatarini zaidi.”

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya WFP, mchanganyiko wa migogoro ya muda mrefu, majanga yanayotokana na hali ya hewa yanayochochewa na mabadiliko ya tabianchi, pamoja na misukosuko ya kiuchumi, utaendeleza ongezeko la njaa na umaskini wa chakula ifikapo mwaka 2026.

Mkazo katika teknolojia, ubunifu na ushirikiano

WFP inasema itazidisha matumizi ya teknolojia na ubunifu ili kuboresha kasi ya utoaji msaada, kupunguza gharama na kuongeza ufanisi. Shirika pia litaimarisha ushirikiano na sekta binafsi ili kuleta suluhisho za ubunifu zenye matokeo ya kudumu.

Mbali na kutoa misaada ya dharura, WFP itaendelea kusaidia jamii kujenga uwezo wa kukabiliana na mishtuko inayotokana na uhaba wa chakula na kuziimarisha serikali kuboresha mifumo yao ya ndani ya usimamizi wa chakula na lishe.

Familia moja imeketi nje ya hema katika kambi ya watu waliokimbia makazi yao huko Jubalan, Somalia.

© WFP/Arete/Mahad Said

Familia moja imeketi nje ya hema katika kambi ya watu waliokimbia makazi yao huko Jubalan, Somalia.

Wito wa hatua na ufadhili wa kudumu

McCain amesema WFP ni msaada muhimu kwa watu wanaoathiriwa na migogoro, mafuriko, ukame na majanga mengine ya mabadilikoyatabianchi, lakini mafanikio ya juhudi hizo yanategemea kujitolea kwa jumuiya ya kimataifa.

Kumaliza njaa sugu kunahitaji ufadhili wa kuaminika na ushirikiano wa dhati,” amesema. “Dunia inaweza kuzuia kuenea kwa njaa, lakini ni lazima tuchukue hatua sasa,” ameongeza.

WFP imezitaka nchi wafadhili na washirika wa maendeleo kuongeza uwekezaji katika programu zilizothibitishwa ili kuzuia kuongezeka kwa njaa na kufanikisha safari ya kuelekea dunia isiyo na njaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *