
Licha ya kauli za Waziri wa Mambo ya Nje wiki iliyopita akizungumzia “usumbufu wa kawaida kwa usambazaji wa mafuta” nchini, raia wanaendelea kuteseka kutokana na kizuizi cha uagizaji wa mafuta kilichowekwa na wanajihadi wa JNIM mapema mwezi Septemba.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wakati malori ya mafuta chini ya uangalizi wa kijeshi yanafanikiwa kupenya na kuepuka mtego wa wanajihadi na kutoa mfano wa “huduma ya chini kabisa,” shughuli bado zinafanyika kwa mwendo wa kinyonga, na nje ya mji mkuu wa Mali Bamako, uhaba unaendelea.
“Hali ni shwari, na kila kitu kinake,da vizuri,” “kuna shughuli zinafanyika kama kawaida”: Wakazi wa Bamako waliowasiliana na RFI wanathibitisha kwamba uboreshaji mdogo ulioonekana katika siku kumi zilizopita unaendelea.
Malori ya mafuta yameweza kufika mji mkuu na polepole yanaondoka katika ofisi za forodha zilizoko katika eneo la uwanja wa ndege, ili kusimamia zoezi la kuhifadhi mafuta kwa muda mrefu.
Kwa hivyo, mamlaka ya mpito iliweza kuandaa maonyesho yao ya kwanza ya biashara iliyojitolea kwa tasnia ya ulinzi: “Bamex” iligonga vichwa vya habari katika vyombo vya habari vya serikali kwa siku kadhaa.
Kusubiri usiku kucha
“Kwenye televisheni, wanatuambia vituo vya mafuta vimefunguliwa, lakini sivyo ninavyoona,” anasema mkazi wa mji mkuu, mwenye hasira, ambaye anadai bado ana ugumu mkubwa wa kujaza tanki lake. “Bado kuna vituo vingi vimefungwa,” anaongeza mwingine, huku wa tatu akisimulia kwamba “watu bado wanafanya usiku kucha wakisubiri kwenye foleni.”
“Tumeamua kuachia ngazi, tumekata tamaa,” anabainisha mkazi wa Bamako kwa uchungu. Kulingana na shuhuda zilizokusanywa, biashara inaendelea polepole kutokana na ugumu wa usafiri na ukosefu wa mafuta kwa kuhudumia jenereta wakati umeme unapokatika.
Katika mikoa, uhaba unaendelea. Huko Ségou, “mistari inaenea kwa kilomita” mbele ya vituo vichache vilivyo wazi, anashuhudia mkazi anayeelezea kwamba, karibu vituo vyote vya mafuta vya jiji, “hakuna hata foleni tena kwa kuwa hakuna mafuta zaidi.” “Hali imezidi kuwa mbaya,” anathibitisha mkazi mwingine wa Ségou, huku akikata tama, kuwa hali inaweza kuwa mbaya zaidi. Huko Koutiala, “vituo vyote viko tupu” anaripoti mkazi mmoja, “tunapata mafuta yetu kwenye soko lisilo kuwa rasmi.”
Kulingana na wakazi kadhaa, meli za mafuta zimewasili Mopti hivi karibuni, lakini yanakwenda kwa jeshi pekee. “Vituo vyetu vya mafuta bado havina watu, na bado hatujapata umeme kwa siku 40,” analalamika mtu maarufu mjini humo. “Hakuna petroli kwa watu; hakuna vituo vilivyo wazi,” analalamika mwingine, ambaye anatarajia “hii itaendelea.” Huko Sikasso, waliohojiwa wanaelezea “foleni ndefu sana katika vituo vichache vinavyouza petroli.” “Niliweza kujaza jana usiku,” mkazi wa Sikasso anasema, akiwa amefarijika kwamba ilibidi asubiri kidogo kuliko kawaida.
Hakuna Kizuizi
Mamlaka ya mpito ya Mali mara kwa mara hudai kwamba wanafanya kazi ili kuhakikisha usambazaji wa mafuta nchini. Lakini pia wanaendelea kukataa kuwepo kwa kizuizi cha wanajihadi huku wakiwashutumu “wafadhili wa kigeni” kwa kujipanga kwa kuunga mkono makundi ya kigaidi, kulingana na taarifa za hivi karibuni za umma zilizotolewa na mawaziri kadhaa katika serikali ya mpito.