Katika eneo la Tawila huko Korma Darfur nchini Sudan kumejengwa kambi ya wakimbizi wa ndani kuhifadhi wale wanaotoka maeneo mbalimbali kukimbia vita inayoendelea nchini mwao.

Ni eneo kame, kuna shida ya maji hapa, watoto wakionekana maeneo ya nje huku wengine wakiwa wamekalia madumu ya maji yaliyo tupu, wanasaka maji.

Huyu ni Sumaya, alikimbia kutoka El Fasher kuja hapa kambi ya wakimbizi wa ndani ya Naira Twila.

“Walituzingira kila kona. Walikuwa wanalenga vyanzo vya maji, masoko na viwanda vya kusaga. Hakuna chakula kinachoweza kuingia wala kutoka. Zile ndege zisizokuwa na rubani zilikuwa zinazunguka muda wote juu katika vichwa vyetu, na kulikuwa na kila aina za silaha juu na ardhini.”

Ndani ya hela amekaa mama huyu aitwaye Halima naye anasimulia aliyopitia anasema “tulipokuwa El Fasher tulipigwa mabomu, watoto wetu wakafa na vijana wametoweka.”

Halima anaendelea kusimulia kuwa “Tulikuwa tukisikia mabomu yakifyatulia juu ya vichwa vyetu, ndege zisizokuwa na rubani na kila aina ya silaha. Na ukienda sokoni basi ujue mtoto wako hatarudi nyumbani na tukisema tuende madukani tu hakuna kitu.”

Mwanamke mwingine aliyekimbia El Fasher ni Haseena ambaye alikuwa mwalimu wa kiingereza na hapa anasimulia.

“Nimekuja na miguu. Tumeteseka sana huko El Fasher. Hali ilikuwa mbaya sana. Hatari sana. Tunaishi kwa hofu. Mwanangu mkubwa alikufa tarehe16 Septemba, alikuwa na umri wa miaka 23. Mwanangu mwingine, mguu wake ulivunjika. Tunataka Kwenda Tawila ili tukamuone daktari, ili afanyiwe upasuaji”

Kilio cha wanawake wote hawa ni kimoja, Amani irejee Sudan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *