Jeshi la DRC FARDC limethibitisha mnamo Novemba 19, 2025, kutekwa kwa mji wa Katoyi na kundi la waasi la AFC/M23, ambalo linadhibiti eneo kubwa mashariki mwa nchi hiyo, hususan katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini. Vikosi vya jeshi la DRC pia vinalaani kitendo hiki kama ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano, ingawa Kinshasa na kundi hili la kisiasa na kijeshi walisaini makubaliano ya mfumo huko Qatar mnamo Novemba 15, hatua kuelekea makubaliano ya amani.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kundi la wanajeshi la AFC/M23 linaendelea na mashambulizi yake huko Kivu Kaskazini, licha ya kusainiwa kwa makubaliano ya mfumo na serikali wiki iliyopita huko Doha.

Siku ya Jumanne jioni, wapiganaji wa AFC/M23 walichukuwa udhibiti wa mji ulioko takriban kilomita 100 magharibi mwa Goma, mji mkuu wa mkoa. Jeshi la Kongo limethibitisha habari hiyo siku ya Jumatano.

Wapiganaji wa kundi la kisiasa na kijeshi waliuteka mji wa Katoyi siku ya Jumanne jioni, baada ya mapigano ya siku moja na jeshi la Kongo, likisaidiwa na wanamgambo wa Wazalendo.

Jeshi la Kongo limethibitisha kutekwa kwa mji huu katika eneo la Masisi, likiishutumu AFC/M23 kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosainiwa Qatar kwa kuanzisha mashambulizi mengi dhidi ya ngome zake katika maeneo ya Walikale, Masisi, na Rutshuru.

Kulingana na mkuu wa eneo la Katoyi, Tshisengele Bazungu Jacque, mapigano ambayo yamekuwa yakiendelea tangu mwanzoni mwa wiki yamesababisha watu wengi kuhama makazi yao.

Je, kambi ya Ntongo kulengwa na mashambulizi ya AFC/M23?

Kutekwa kwa Katoyi kunakuja baada ya kuanguka kwa maeneo mengine kadhaa huko Masisi: Kazinga, Kasheke, na Bibatama. Kulingana na vyanzo vya utawala, kundi hilo lenye silaha linatafuta kufika katika mji wa Ntongo, kilomita 40 kutoka hapa, ambapo kambi kubwa ya jeshi la Kongo inapatikana.

Mapigano zaidi pia yameripotiwa kaskazini zaidi katika eneo la Lubero, na pia katika mkoa jirani wa Kivu Kusini, ambapo mapigano yalizuia kwa muda shughuli mbalimbali siku ya Jumatano asubuhi kwenye barabara ya Bukavu-Walungu mjini

Kinshasa na AFC/M23 walisaini tamko la kanuni huko Doha mnamo mwezi Julai kwa niaba ya “usitishaji mapigano wa kudumu,” ambao haujamaliza mapigano. Siku ya Jumamosi, pande hizo mbili zilisaini makubaliano mapya, Mfumo wa Doha wa Mkataba Kamili wa Amani, katika sherehe iliyohudhuriwa na maafisa kutoka pande zote mbili, pamoja na wapatanishi wa Marekani na Qatar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *