
Wiki iliyopita, boti moja ilionekana pwani ya Mauritania baada ya kuondoka kutoka maji ya Gambia na kuelea kwa karibu wiki mbili baharini. Watu wengi hawajulikani walipo, wengi wao kutoka Conakry. RFI imeenda kukutana na baadhi ya familia zilizofiwa katika kitongoji cha Bonfi, nje kidogo ya mji mkuu wa Guinea, Conakry.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Conakry, Mouctar Bah
Machozi, hisia, na huzuni vimejaa maeneo ya wakaazi wa maeneo yenye watu wengi ya Bonfi. Hapa ndipo msafara wa wahamiaji haramu uliondoka. Issiagha Camara ndiye msemaji wa waathiriwa, ambao wameunda chama chao anasema “mnamo tarehe 13 (Novemba), kijana mmoja alimpigia simu dada yake mkubwa, akilia, akisema, ‘Walituua, walituua.'” Alipotoa taarifa hiyo, kila mtu alitaka kujua kinachoendelea.
Kati ya mamia ya watu wanaodhaniwa kutoweka, majina ya vifo vilivyothibitishwa yanaingia kwenye simu, moja baada ya jinngine. “Kuna vifo saba vilivyothibitishwa rasmi nchini Guinea,” anaelezea Issiagha Camara. “Wazazi hao wako hapa; wanaweza kutoa ushuhuda. Huyu ni mtu wa saba ambaye tumempokea.”
Leo, hakuna anayejua ni watu wangapi walikuwa ndani ya boti hiyo. Ousmane Yansané, kiongozi wa CLEF, Baraza la Watoto na Familia katika eneo hilo, anasema:
“Wanasema kulikuwa na zaidi ya watu 400, wengine wanasema 300 hivi, waliokuwa ndani ya boti hiyo kutoka Gambia, lakini watu hao 300 wote sio Waguinea. Wako huko katika hali ngumu, wanalia, wanataka kurudi Guinea, lakini vipi?” Tunaomba serikali, kupitia Wizara ya Mambo ya Nje, itusaidie kuwaleta vijana hawa nyumbani.
Mwaka jana katika kipindi kama hiki, vijana 34 kutoka eneo hili hilo walifariki wakijaribu kuingia katika Visiwa vya Canary.