
Kesi ya Roger Lumbala inaendelea katika mahakama moja ya mjini Paris, mji mkuu wa Ufaransa, ingawa amekataa kufikishwa mahakamani tangu kesi ilipoanza Novemba 12. Mbabe huyo wa zamani wa kivita nchini DRC anashtakiwa nchini Ufaransa kwa kushiriki katika uhalifu wa kivita chini ya kanuni ya mamlaka ya ulimwengu.
Imechapishwa:
Dakika 3 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Luc Henkinbrant, afisa wa zamani wa haki za binadamu aliyeanzisha uchunguzi wa ripoti Mapping, iliyochapishwa mwaka wa 2010, amekuja kuelezea yaliyomo katika hati hii ya Umoja wa Mataifa. Hati hiyo iliyotumwa baada ya kugunduliwa kwa kaburi la watu wengi mwaka wa 2005, inaorodhesha uhalifu dhidi ya ubinadamu uliofanywa kati ya mwaka 1993 na 2003 katika eneo hilo.
Luc Henkinbrant, afisa wa zamani wa haki za binadamu ambaye kwa sasa ni mstaafu, alihojiwa kuhusu Ripoti ya Mapping mnamo Novemba 19, 2025, huko Paris. Jaji aliyeongoza kesi alisoma dondoo kadhaa, haswa zile zinazohusiana na Operesheni “Futa ubao”: “Angalau raia 373, wakiwemo Mbilikimo, waliuawa.” Aliongeza: “Wanamgambo kutoka mkoa wa Kivu Kusini pia wanadaiwa kukusanya majimaji ya uke ili kutengeneza vitu vya kichawi. Wanachama wa MLC na RCD-N pia wanaripotiwa kutengeneza hirizi kwa kutumia sehemu za siri zilizovutwa.”
Luc Henkinbrant alithibitisha kwamba taarifa hii ilijumuishwa katika Ripoti ya Mapping. Afisa huyo wa zamani wa haki za binadamu alihitimisha ushahidi wake na kuipongeza Mahakama kwa kuchukua kesi hiyo na kuruhusu waathiriwa kusikilizwa.
Hata hivy, siku ya Jumatano aligundua, wakati wa vikao, kwamba Mahakama ya Paris haikuwa imepewa ruhusa ya kufikia viambatisho vya Ripoti ya Mapping, ambavyo vina majina ya wahusika wanaodaiwa wa uhalifu dhidi ya binadamu uliofanywa kati ya mwaka 1993 na 2003. Kulingana na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, viambatisho hivi vitapatikana ikiwa mahakama itaviomba.
“Ni kashfa halisi ambapo hifadhidata hii haijafichuliwa,” ametangaza
“Ni kashfa halisi ambapo hifadhidata hii, ambayo ina majina ya wahusika wanaodaiwa wa uhalifu huu, haijafichuliwa mpaka sasa, mbele ya Mahakama hii.” Wengi wa wahalifu katika hifadhidata hii, wahalifu wa uhalifu huu, ni watu wa ngazi ya juu ambao wanaweza kuwa na nguvu za kisiasa na kijeshi nchini DRC, lakini pia katika nchi jirani kama Uganda na haswa Rwanda, nchi jirai, ambayo kwa hivyo inafaidika na kutumia makundi haya waasi wa Kongo. Hii ni vita ya kiuchumi inayoiwezesha kuchimba maliasili: madini, dhahabu, ambayo hupatikana haswa katika maeneo ambayo RCD-N na mshirika wake, MLC, inayoungwa mkono na Uganda, walitaka kudhibiti.
Wakati huo huo katika taarifa iliyosomwa siku ya Jumatano asubuhi na jaji mkuu, kiongozi huyo wa zamani wa waasi aliomba kushtakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.
Roger Lumbala alikamatwa mwezi Desemba 2020, akafanyiwa uchungzi Januari 4, 2021, na kushtakiwa mwaka 2023. Amekuwa akishtakiwa tangu Novemba 12, 2025, huko Paris, mbele ya Mahakama, kwa kushiriki katika uhalifu dhidi ya ubinadamu na njama ya kutenda uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa vitendo vilivyofanywa mashariki mwa DRC, haswa mwaka 2002. Kwa sasa anashtakiwa chini ya kanuni ya mamlaka ya ulimwengu. Hii ni kesi ya kwanza nchini Ufaransa inayomhusisha raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kuanzia Novemba 12 hadi Desemba 19, 2025, jaji mkuu wa Mahakama ya Assize na naibu waendesha mashtaka wawili wa kupambana na ugaidi watachunguza jukumu la kiongozi huyu wa zamani wa waasi wa RCD-N, anayetuhumiwa kushiriki katika Operesheni “Futa ubao” pamoja na Naibu Waziri Mkuu wa sasa wa DRC na kiongozi wa zamani wa waasi Jean-Pierre Bemba, ambaye wakati huo alikuwa kiongzi wa kundi la waasi la MLC. Operesheni hii iligubikwa na mauaji ya halaiki, ubakaji, na vitendo vya mateso, haswa dhidi ya raia kutoka jamii ya Batwa na Nande. Roger Lumbala hakuwahi kushtakiwa.
Zaidi ya miaka ishirini baada ya matukio hayo, kesi hii ya mfano inategemea ripoti na ushuhuda mbalimbali kutoka kwa waathiriwa huko Haut-Uélé na Ituri. Kwa vyama vya kiraia, inawakilisha hatua ya kihistoria mbele dhidi ya kutokujali; kwa upande wa utetezi, shambulio dhidi ya uhuru wa Kongo.