Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imesema kuwa zaidi ya watu 1,900 waliuawa katika mashambulio 450 ya kigaidi yaliyorekodiwa Afrika Magharibi katika mwaka huu.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa rais wa jumuiya ya ECOWAS, Omar Alieu Touray, wakati wa majadiliano ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika mapambano dhidi ya ugaidi kwenye eneo la Afrika Magharibi na Sahel, amethibitisha ripoti hiyo.

Kwa mujibu wa Ecowas makundi yenye itikadi kali pia yameonekana kujitosa kwenye vita vya kiuchumi kwa  kuzuia upatikanaji wa mafuta na kufunga baadhi ya barabara hali iliyosababisha jumuiya hiyo kuongeza vikosi vyake kutoka maafisa   1,650 na hadi 5,000.

Mnamo Januari 29, 20205 Burkina Faso, Mali na Niger zilitangaza rasmi kujiondoa kutoka kwa jumuiya hiyo zikishtumu mataifa washirika kutumiwa na mataifa ya kigeni, ikiwa ni pamoja na Ufaransa.

Mbali na nchi hizi tatu, nchi nyingine za Afrika Magharibi Benin, Ivory Coast, Nigeria na Togo zinakabiliwa na mashambulizi ya kigaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *