
Hali ya wasiwasi imezidi kushuhudiwa katika maeneo kadhaa ya Masisi,Kivu Kaskazini ,nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,maeneo yanayokaliwa na waasi wa AFC/M23 ambapo kumeshuhudiwa mapigano kati ya waasi hao na jeshi la Congo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Baada ya mapigano ya siku tatu kati ya waasi wa AFC/M23 na FARDC kwa ushirikiano na wapiganaji wazalendo, maeneo mengi mapya yanadhibitiwa na waasi wa M23, kuanzia Kasheke, Bitunu na Katayo yaliyotekwa tangu siku ya Jumapili na Jumanne wiki hii.
Kwa upande mwingine vijiji vya Kashanje na Nyampanika katika eneo la Mweso ,sasa vinadhibitiwa na wapiganaji Wazalendo.
Mapigano hayo yamefanya hali ya kibinadaam kuwa mbaya huku wakaazi wakiendelea kuyakimbia makazi yao kuhofia kuuawa.
Mashirika ya kiraia kwenye eneo la Masisi ,yamelaani kampeni ya waasi wa M23 kuweka utawala mbadala katika maeneo hayo ,hii ikijiri baada ya makubaliano yaliyosainiwa kati ya mamlaka ya Kinshasa na waasi wa AFC/M23.