Serikali ya Niger, imetangaza kuyafunga mamia ya mashrika ya kiraia ya ndani na yale ya kimataifa yakiwemo pia yale ya misaada, hatua hii ikiwa ni muendelezo wa utawala wa kijeshi kudhibiti shughuli za mashirika yasiyo ya kiserikali nchini humo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tangu jeshi lilipopindua serikali ya kiraia mwaka 2023, kiongozi wa mpito wa kijeshi jenerali Abdourahamane Tiani, amekuwa akiyashutumu baadhi ya mashirika kutokuwa na uwazi pamoja na kuunga mkono harakati za kigaidi kwenye taifa hilo.

Mwezi Januari mwaka huu waziri wa mambo ya ndani, Jenerali Mohamed Toumba, alitangaza muongozo mpya wa shughuli za mashirika ya kiraia, miongozo iliyolenga kudhibiti na kusimamia shughuli za mashirika hayo.

Aidha mwezi uliopita, serikali iliruhusu shughumi za mashirika 100 pekee kati ya elfu nne yaliyokuwa yanafanya kazi nchini humo, serikali ikitaka mashirika ambayo hayajapewa kibali kusitisha shughuli zao.

Niger ina mashirika ya kiraia na yale ya maendeleo zaidi ya alefu 4, yakiwemo 332 ambayo ni ya kigeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *