Nchi ya Uchina Alhamisi ya wiki hii ilisaini makubaliano ya dola bilioni 1.4 na Zambia pamoja na Tanzania ili kuboresha reli ya TAZARA inayounganisha taifa hilo lisilo na Bahari.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Reli hiyo iliyofadhiliwa na China katika miaka ya 1970 kwa lengo la kurahisisha usafirishaji wa bidhaa za shaba na mafuta kupitia Tanzania inasalia kuwa muhimu katika masuala ya kibiashara ya Ukanda.

Aidha inaripotiwa kuwa hatua ya China ni njia moja ya kuleta ushindani wa kibiashara haswa katika mradi wa Lobito unatokea nchini Angola kupitia Zambia hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mradi unaoungwa mkono na Umoja wa Ulaya na Marekani.

Makubaliano kati ya Tanzania, China na Zambia yalitiwa saini wakati za ziara ya Waziri Mkuu wa China Li Qiang jijini Lusaka, ziara yake ya kwanza katika kipindi cha miaka 28. 

Wakati wa hafla hiyo, China ilisisitizia utayari wake wa kushirikiana na Zambia na Tanzania kuhakikisha kwamba mradi wa reli hiyo unafanikiwa na unakuwa na manufaa kwa raia wa nchi hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *