Urusi inasema, hajapokea taarifa zozote rasmi kutoka Marekani, kuhusu pendekezo lolote la mpango wowote kuhusu kumaliza vita vyake na nchi jirani ya Ukraine.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kauli hii ya Moscow imekuja, baaada ya rais Volodymr Zelensky kusema, yupo tayari kushirikiana na serikali ya rais Donald Trump, kuhusu mpango wake wa kumaliza vita vinavyoendelea.
Urusi badala yake, imeendelea kutekekeleza mashambulio mazito Kusini mwa jimbo la Zaporizhzhia na maeneo ya Kusini, siku ya Ijumaa, na kusababisha vifo vya watu watano.

Siku ya Alhamisi ripoti ilivuja, kuhusu mapendekezo ya Marekani, kuwa Ukraine ilikuwa imekubali Urusi kuchukua baadhi ya maeneo ya jimbo la Donestk, kupunguza idadi ya wanajeshi wake na kuachana na mpango wa kujiunga na NATO, ili kupata suluhu ya vita hivyo.
Hata hivyo, washirika wa Ukraine, nchi za Umoja wa Ulaya, zimeendelea kusisitiza kuwa ni lazima zihusishwe kwenye mpango wowote wa kumaliza vita nchini Ukraine.