
Mahakama ya Paris imetoa uamuzi mnamo Novemba 21, 2025, kwamba ina “uwezo wa kumfungulia mashitaka na kumhukumu” kiondozi wa zamani kivita nchini DRC, Roger Lumbala, jaji mkuu amehitimisha baada ya kusoma uamuzi uliokataa pingamizi la upande wa utetezi kuwa mahakama hiyo haina uwezo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 3 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mwasi huyo wa zamani wa Kongo amekuwa akishtakiwa tangu wiki iliyopita kwa kushiriki katika uhalifu dhidi ya binadamu. Anakabiliwa na kifungo cha maisha jela kwa vitendo vya kuanzia mwaka 2002-2003 kaskazini mashariki mwa DRC, wakati wa operesheni iliyopewa jina la “Futa Ubao.” Akiwa kizuizini tangu kukamatwa kwake mnamo Desemba 2020 huko Paris, ameamua kutohudhuria kesi hiyo na amewafukuza mawakili wake.
Roger Lumbala, anayeshtakiwa kwa kushiriki katika uhalifu dhidi ya binadamu na njama za jinai nchini DRC, anaendelea kukataa kufika mahakamani. Mwanzoni mwa kesi mnamo Novemba 12, mawakili wa utetezi walidai kwamba mahakama hiyo ya Ufaransa haina uwezo wa kumhukumu mteja wao. Mshtakiwa mwenyewe alikuwa na ujumbe unaosomwa kwa sauti kila siku ukisema kwamba kanuni za utaratibu wa jinai hazikufuatwa na kwamba ushahidi ulioandikwa kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ulihitajika kuthibitisha kwamba haimfuatilii.
Baada ya kusoma hoja za mshtakiwa mwanzoni mwa kusikilizwa kwa kesi hiyo, jaji mkuu wa Mahakama ya Paris, Marc Summerer, alijibu: ndio, upande wa mashtaka ulikuwa umethibitisha kwamba hati ya kukamatwa ya 2013 iliyotolewa nchini DRC haikuwa na uhusiano na kesi ya sasa. Wakati huo, mshtakiwa alikuwa akishtakiwa kwa uhaini huko Kinshasa. Alikuwa akitafuta hadhi ya ukimbizi wa kisiasa nchini Ufaransa, akiogopa kwamba kesi yake haingeendeshwa kwa uhuru. Na ili kushughulikia dai lingine lililotolewa na mshtakiwa, mamlaka ya Kongo kweli ilitoa hati ya kukamatwa kwa Roger Lumbala mnamo mwezi Juni 2025. Hata hivyo, haiwezekani kumshtaki mtu katika mahakama mbili tofauti kwa kosa moja.
Roger Lumbala alishtakiwa mwaka wa 2021 kwa kushiriki katika uhalifu dhidi ya ubinadamu na njama za jinai, mashtaka ambayo DRC imekuwa ikitoa kwa miezi kadhaa, bila kutoa ushahidi wowote kuunga mkono ombi hili la hivi karibuni, kulingana na uamuzi uliosomwa asubuhi ya Ijumaa.
Jaji mkuu ameongeza: ICC iliarifiwa mwaka wa 2017 kuhusu uchunguzi ulioanzishwa na mamlaka ya Ufaransa. Hata hivo, haijawahi kudai mamlaka yake. Kwa hivyo, mshtakiwa hawezi kudai taarifa ya mamlaka. Mamlaka ya jumla ya Mahakama ya Paris imethibitishwa.
Kwa Henri Thulliez, wakili anayewawakilisha walalamikaji katika kesi hiyo, mjadala kuhusu mamlaka ya jumla hatimaye umekwisha. “Jaji mkuu wa Mahakama ya Paris , Marc Summerer, alikataa ombi la Roger Lumbala la kutaka kufutwa, ambalo alikuwa amewasilisha kabla ya kuwafukuza mawakili wake na kukataa kuhudhuria kesi hiyo.”
Lakini karibu kila siku, licha ya kutokuwepo kwake, mshtakiwa anaendelea kuzua gumzo nje ya mfumo wa mahakama. Mnamo Novemba 21, barua ilisambazwa. Ilisafirishwa kisiri kutoka gereza la La Santé na kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii. Barua hii iliyoandikwa kwa mkono, iliyoelekezwa kwa Rais wa Kongo Félix Tshisekedi na viongozi kadhaa wa zamani wa Movement for the Liberation of Congo (MLC), wanasiasa na wanajeshi ambao bado wana ushawishi, kulingana na Thulliez: “Barua hii inaonyesha kwamba Roger Lumbala anamwomba Jean-Pierre Bemba akubali kutoa ushahidi kupitia njia ya video ili kutoa toleo lake la matukio, bila shaka kwa lengo la kumtoa hatiani.” Ingekuwa bora kutoa kauli kama hiyo mbele ya majaji. Kwa njia hiyo, kusingekuwa na shaka au kusitasita kuhusu asili ya ujumbe huu.”
Daniel Perissi, mratibu wa Trial International nchini DRC, shirika lisilo la kiserikali linalotoa msaada wa kisheria kwa waathiriwa, anarejelea maombi yaliyotolewa katika barua hii kwa wanasiasa kadhaa mjini Kinshasa.
Kuna majina kadhaa yaliyonakiliwa kwenye barua hiyo, ikiwa ni pamoja na lile la Rais Tshisekedi. Labda kuna masuala yanayohusika ndani ya mitandao ya ushawishi ambayo Roger Lumbala bado ana uhusiano nayo nchini DRC.
Je, Roger Lumbala atahudhuria wiki ijayo kuwasikiliza mashahidi na waathiriwa wa Operesheni “Futa Ubao? Swali linabaki kuwa wazi.