Rais wa Ukraine amekutana na Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance siku ya Ijumaa kujadili mpango wa kukomesha vita. Hapo awali, alifanya mashauriano ya dharura na viongozi wa Ufaransa, Ujerumani, na Uingereza. Mkataba huo wa Marekani wenye pointi 28 unaitaka Kyiv ikubali kupoteza maeneo yanayokaliwa na Urusi, kutojiunga na NATO, ipunguze vikosi vyake vya jeshi, na ifanye uchaguzi mara baada ya hapo. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba kwa taifa, ambayo video yake ilirushwa kwenye mitandao ya kijamii, Volodymyr Zelensky amehakikishia uma kwamba hataisaliti Ukraine, lakini kwamba nchi yake inaweza kukabiliwa na chaguo gumu sana: “ama kupoteza utu, au hatari ya kupoteza mshirika mkuu.” 

Washington inaweka shinikizo kubwa kwa Ukraine na, kulingana na shirika la habari la Reuters, inatishia kuacha kushiriki taarifa za kijasusi na kusimamisha kuipa silaha Ukraine ikiwa haitasaini makubaliano ya amani ifikapo Alhamisi, Novemba 27.

Wakati huo huo Rais wa Marekani Donald Trump alisema Zelensky “hana budi kukubali” mpango huo, na kuongeza kuwa vinginevyo Ukraine na Urusi zitaendelea kupigana.

Katika mkutano wa Ijumaa na baraza lake la mawaziri la usalama, Putin alisema Moscow imepokea mpango huo, ambao haujajadiliwa kwa kina na Kremlin. Alisema Urusi ilikuwa tayari “kuonyesha kubadilika” lakini pia iko tayari kupambana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *