Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, Volker Turk, amelalamikia kile alichokisema makubaliano finyu ya mkutano wa hali ya hewa COP30 uliomalizika juma lililopita nchini Brazil, akionya kuwa viongozi kushindwa kuchukua hatua stahiki siku moja matendo yao yatatafsiriwa kuwa uhalifi dhidi ya binadamu.

Mkutano wa mazingira wa COP30 ulifanyika jijini Belem nchini Brazil.
Mkutano wa mazingira wa COP30 ulifanyika jijini Belem nchini Brazil. REUTERS – Adriano Machado

Matangazo ya kibiashara

Jumamosi iliyopita mataifa yalikubaliana kimsingi kuhusu mkataba wa hali ya hewa wa COP30 baada ya majadiliano magumu, mkataba ambao hata hivyo haukutoa suluhu ya moja kwa moja kuhusu namna nchi zitaanza kuachana na matumizi ya mafuta Visukuku.

Akihutubia kongamano la Umoja wa Mataifa la biashara na haki za binadamu, Turk ameonya kuwa makubaliano yaliyofikiwa yanaonesha namna makampuni yenye nguvu yanaushawishi katika kupunguza kasi ya kudhibiti athari za tabianchi.

Turk amesema mataifa na makampuni yanayozalisha mafuta kwa wingi wameendelea kupata faida maradufu huku athari kubwa za mabadiliko ya tabia nchi zikibebwa na jamii kutoka nchi masikini, akitaka uwajibikaji kwa madhara yenye kuhusu hali ya hewa.

Kusambaza :

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *