Katika kituo cha Club inayofahamika kwa jina Itihad Shabab Deir al-Balah, kwenye mji wa Deir al-Balah, katikakati mwa Ukanda wa Gaza, vijana wanaonekana wakijiandaa kucheza mpira wa miguu japokuwa wengi wao wana mguu mmojammoja na wanatumia magongo kutembea.
Bango linaeleza waziwazi, michuano ya matumaini ya Mpira wa Miguu kwa watu waliokatwa viungo katika Ukanda wa Gaza.
Kapteni Ali Abu Armanah, kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Palestina na mratibu wa mradi katika Chama cha Soka cha Walemavu wa Kipalestina.
Ali Abu Armanah, Nahodha wa timu ambaye pia ni Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Soka la Watu Waliokatwa Viungo Palestina pia akiwa ndiye Mratibu wa Mradi, Chama cha Soka cha Watu Waliokatwa Viungo Palestina anasema, “tumekuja kwenye mashindano haya kurejesha matumaini baada ya miaka miwili ya vita vya mauaji vilivyolengwa dhidi yetu na watu wetu katika Ukanda wa Gaza. Kwa wakati huu mahsusi, tulipaswa kuwa Jakarta – Indonesia – kuiwakilisha Palestina katika mashindano ya kufuzu katika Asia Magharibi kwenda Kombe la Dunia la mwaka 2026, ambalo litafanyika Costa Rica. Hata hivyo, kufungwa kwa kivuko na vita kumezuia ushiriki wetu.”
Kwa upande wake Abdullah Abu Mukhaimer, mchezaji, Timu ya Taifa ya Soka la Watu Waliokatwa Viungo Palestina anasema, “ninataka kufikisha ujumbe wangu kwamba tunaendelea kujitolea na kuipenda soka hapa Ukanda wa Gaza. Sasa kuna majina mapya mengi, kwani kuna takribani watu 60,000 waliokatwa viungo Gaza kutokana na vita vya hivi karibuni. Tutaendelea, na tunatumaini mamlaka husika zitatoa kipaumbele kwa soka la watu waliokatwa viungo Gaza kwa sababu idadi yao ni kubwa sana.”
Farah Youssef, mchezaji wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Palestina, ambaye anashiriki michuano hiyo.
Sio wanaume tuna wanawake nao wamo. Farah Youssef anasema,
“Nimekuja hapa kucheza na kujaribu kurejesha uwezo wangu kama ilivyokuwa kabla ya vita na kufufua kumbukumbu zangu. Ujumbe wangu kwa wale walio kama mimi: msikate tamaa. Songa mbele. Licha ya jeraha na kukatwa kiungo, endeleeni kusonga.”
Wachezaji wengi wanaoshiriki katika timu za michezo ya watu waliokatwa viungo walijeruhiwa katika vita na operesheni za kijeshi katika miaka iliyopita katika Ukanda wa Gaza.
Mohammed Abu Joufil, ambaye alijeruhiwa katika vita vya 2014 dhidi ya Gaza, akijiandaa kushiriki michuano ya Hope kwa kandanda ya watu wasio na viungo.
Muhammad Abu Joufil, aliyejeruhiwa katika vita ya mwaka 2014 humo humo Gaza, naye ni mshiriki wa mashindano haya ya tumaini ya soka la watu waliokatwa viungo anasema, “nilikuwa nikicheza soka kabla ya kujeruhiwa, na baada ya mguu wangu kukatwa nilikaa bila kufanya chochote kwa kama miezi mitano. Klabu niliyokuwa nikichezea ilinijulisha kwamba kulikuwa na klabu maalum kwa watu waliokatwa viungo. Nilienda, na mwanzo ulikuwa mgumu; nilikuwa nimezoea kucheza nikiwa na miguu miwili, sasa mguu mmoja na magongo. Tulifundishwa bila kukoma kwa miaka miwili, na tukakutana na mchezaji aliokatwa kiungo kutoka nje ya nchi ambaye alitupa ushauri na kutusaidia. Baada ya hapo, tuliendelea na maisha yetu.”