Akizungumza nchini Angola, ikiwa ni wiki chache kabla ya kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wake, Guterres amezitaka bara mbili hizo kuwa “mhimu wa kifungu cha enzi mpya ya ulimwengu wa kimataifa, unaojengwa juu ya ushirikiano badala ya mgawanyiko. “

Amesema “Kinyume na kugawanyika kwa dunia katika kambi mbili, tunahitaji ulimwengu wa wenye mshikamano wa kimataifa ulio na mtandao mpana wa mahusiano. Lakini ushirikiano wa kimataifa pekee si dhamana ya amani.”

Bi. Charlotte Lusenge mfanya biashara Beni-DRC pia munufaika wa pesa kutoka Umoja Wa Mataifa kupitia MONUSCO. Alifanikiwa na msaada baada yakupoteza biashara yake wakati soko la Mayangose lilipo ungua januari.

UN News/George Musubao

Bi. Charlotte Lusenge mfanya biashara Beni-DRC pia munufaika wa pesa kutoka Umoja Wa Mataifa kupitia MONUSCO. Alifanikiwa na msaada baada yakupoteza biashara yake wakati soko la Mayangose lilipo ungua januari.

Mifumo ya fedha haina uadilifu

Katika hotuba yake Guterres ametaja maendeleo endelevu kuwa kipaumbele cha kwanza, akikosoa vikali mfumo wa sasa wa fedha duniani ambao ameuita “usio sawa na usio na ufanisi, na unaopendelea mataifa tajiri tayari.“

Amewataka viongozi kuunga mkono mageuzi makubwa, ikiwemo kukomesha “mzunguko wa madeni unaobana koo nchi masikini, kuongezwa mara tatu kwa uwezo wa kukopesha wa benki za maendeleo za kimataifa, na kuongeza ushiriki wa nchi zinazoendelea hasa zile za Afrika katika taasisi za kifedha za dunia.”

Amewachagiza kuwa “Pamoja, mnaweza kukomesha dhuluma ya umaskini na kufungua uwezo mkubwa wa kiuchumi wa bara hili”.

Rasilimali za Afrika ziwafaidi Waafrika

Akigeukia hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, Guterres ametilia mkazo utajiri wa Afrika katika jua, upepo na madini muhimu mali ambazo amesema zitahitajika mara tatu zaidi kufikia 2030 kutokana na mabadiliko ya dunia kuelekea nishati safi.

Lakini ameonya dhidi ya kurudia mifumo ya zamani ya unyonyaji wa rasilimali iliyowaacha Waafrika bila manufaa. “Hii lazima iwe fursa ya kukataa mifano ya zamani ya uchimbaji usio na thamani ya ndani,” amesema, akitaka uchakataji na uzalishaji ufanyike barani Afrika.

Amezitaka nchi tajiri kutimiza ahadi zao za ufadhili wa tabianchi, ikiwemo kuongeza ufadhili wa kukabiliana na athari za tabianchi hadi angalau dola bilioni 40 mwaka huu na kuutrilisha kufikia 2035.

“Kwa mafunzo sahihi na ufadhili, mageuzi ya nishati mbadala yanaweza kulitendea haki bara zima,” amesema.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres (kushoto) akikutana na viongozi nchini Angola wakati wa mkutano wa Muungano wa Afrika.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres (kushoto) akikutana na viongozi nchini Angola wakati wa mkutano wa Muungano wa Afrika.

Ufadhili wa uhakika kwa ajili ya amani

Akigusia migogoro inayoendelea duniani, Guterres amelaani mateso yanayosababishwa na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine na ghasia zinazoendelea nchini Sudan, Sudan Kusini, Somalia, Libya, Mali na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

Amewataka viongozi kuunga mkono Mkataba wa Zama Zijazo uliopitishwa mwaka jana, unaojumuisha viti vya kudumu kwa Afrika katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. “Hili litarekebisha dhuluma ya kihistoria,” amesema, akiongeza kuwa litafanya Baraza kuwa lenye ufanisi zaidi.

Amesisitiza tena wito wake wa ufadhili “endelevu, unaobadilika na wa kutabirika kwa operesheni za amani zinazoongozwa na AU”, akiushukuru Muungano wa Ulaya kwa uungwaji mkono wa miaka mingi.

AU na EU zina nguvu ya kuiongoza dunia

Kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa amewakumbusha viongozi kwamba pamoja, Muungano wa Afrika na Muungano wa Ulaya wanawakilisha asilimia 40 ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa uzito wa kisiasa unaoweza kusukuma mbele sheria za kimataifa, kufanikisha makubaliano na kuunda utawala wa dunia.

“Mna uwezo wa kulinda Katiba ya Umoja wa Mataifa na kuielekeza dunia katika uhalisia thabiti na shirikishi zaidi,” amesema.

Ameonya kwamba katika mazingira ya sasa ya nguvu za kimataifa kubadilika, taasisi thabiti za kikanda na kimataifa ni muhimu ili kuzuia machafuko na migogoro mikubwa.

Wito wa enzi mpya ya matumaini

Guterres amehitimisha ujumbe wake kwa wito wa umoja katika kipindi ambacho amekitaja kuwa chenye misukosuko lakini pia chenye fursa.

“Kutoka kwenye misukosuko ya leo, mnaweza kuunda enzi mpya ya matumaini,” amesema, akihimiza AU na EU kujenga dunia ambayo “udhalimu na ukosefu wa usawa vinatokomezwa hatua kwa hatua.”

Ujumbe wake wa mwisho umekuwa wito wa ushirikiano wa kina kati ya mabara hayo mawili “Kwa umoja. Kwa usawa. Na kwa amani.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *