
Amnesty imesema imekusanya ushahidi kutoka kwa manusura 28 walioelezea ukatili huko El-Fasher kuanzia mauaji ya kushtukiza ya wanaume wasio na silaha hadi ubakaji wa wasichana na wanawake.
Mkuu wa Amnesty Agnes Callamard amesema kwenye ripoti iliyochapishwa hii leo kwamba “Ukatili dhidi ya raia unaweza kuwa uhalifu wa kivita ama uhalifu mwingine chini ya sheria ya kimataifa na kutaka wahusika kuwajibishwa.
Aidha ameiomba jumuiya ya kimataifa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuitaka UAE kuacha kuwaunga mkono RSF, licha ya taifa hilo kukanusha mara kwa mara madai hayo.