
Leo, Novemba 25, ni Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake. Nchini Côte d’Ivoire, serikali imerekodi zaidi ya visa vya ubakaji 1,200 na unyanyasaji wa kingono ambao ulishughulikiwa katika ngazi ya kitaifa mwaka wa 2024. 12% ya kesi hizi zilirekodiwa katika wilaya ya Abidjan pekee, lakini unyanyasaji wa kijinsia pia ni tatizo nje ya jiji hili kubwa zaidi la Côte d’Ivoire.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu mjini Abidjan, Benoit Almeras
Zaidi ya kesi 150 za visa vya ubakaji. Hiyo ndiyo idadi ya kesi zilizoshughulikiwa katika mamlaka ya Mahakama ya Rufaa ya Korhogo, kaskazini mwa Côte d’Ivoire, kwa kikao cha mwaka 2024/2025 pekee. Mamlaka za mahakama huko Korhogo zimetaka uhamasishaji wa mkubwa.
Nje ya Abidjan, serikali ilirekodi karibu visa 10 vilivyoripotiwa vya ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia kwa kila wanawake 100,000 mwaka wa 2024, kiwango ambacho ni mara mbili zaidi ya Abidjan, kulingana na kitabu cha takwimu cha Wizara ya Wanawake na Watoto.
Kulingana na shirika linalotetea Haki za Wanawake nchini Côte d’Ivoire, waathiriwa mara nyingi hushindwa kuwasilisha malalamiko, haswa katika maeneo ya vijijini. Hii inatokana, kulingana na Marie Bénédicte Kouadio, mkuu wa idara ya sheria ya shirika hilo, na tatizo la umbali wa ofisi za polisi, lakini si hivyo tu.
“Ni vigumu kwao kuchukua hatua ya kwanza, kwenda polisi na kuwasilisha malalamiko. Kisha, kuna suala muhimu la elimu kuhusu kuwasilisha malalamiko. Wanawake hawa wanapokuwa waathiriwa wa ukatili huu, wazo lao la kwanza si kuripoti mshambuliaji wao; wengine hawajui hata wana haki ya kuripoti, kwamba wako ndani ya haki zao.”
Ili kuwasaidia waathiriwa, serikali imeanzisha majukwaa 95 kote nchini ili kupambana na vurugu zinazotokana na jinsia. Kulingana na mkurugenzi wa programu hii ya kitaifa, kampeni endelevu za uhamasishaji umma ni muhimu. Serikali ya Côte d’Ivoire pia imewataka raia kupiga simu bila malipo kupitia namba, 1308, ili kuwaelekeza waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia kwa huduma zinazofaa.