“Kuokoka kwa Gaza kumo hatarini,” Umoja wa Mataifa umeonya katika ripoti ya leo Jumanne, Novemba 25, 2025, ukiitaka jumuiya ya kimataifa kuunda “mpango kamili wa uokoaji” na kuingilia kati “bila kuchelewa” na kwa njia iliyoratibiwa.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Operesheni za kijeshi za Israel huko Gaza “zimeharibu nguzo zote za kuishi,” kuanzia chakula na malazi hadi huduma ya afya, “zimedhoofisha utawala na kutumbukiza” eneo la Palestina “katika shimo lililotengenezwa na mwanadamu,” inalaani ripoti kutoka Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Biashara na Maendeleo (UNCTAD).

“Kwa kuzingatia uharibifu usiokoma na wa kimfumo huko Gaza, kuna mashaka makubwa kuhusu uwezo wa Gaza wa kujijenga upya kama nafasi wtu wanayoweza kuishi na jamii,” ripoti hiyo inaongeza.

Vita huko Gaza vilichochewa na shambulio dhidi ya Israel iliyoendeshwa na Hamas mnamo Oktoba 7, 2023, ambalo lilisababisha vifo vya Waisraeli 1,221, wengi wao wakiwa raia, kulingana na hesabu ya shirika la habari la AFP. Zaidi ya Wapalestina 69,756 waliuawa katika kampeni ya kulipiza kisasi ya kijeshi ya Israel, kulingana na Wizara ya Afya ya Gaza. Data hii, inayochukuliwa kuwa ya kuaminika na Umoja wa Mataifa, haionyeshi idadi ya wapiganaji waliouawa, lakini inaonyesha kwamba zaidi ya nusu ya waliofariki walikuwa watoto na wanawake.

Haja ya “mpango kamili wa uokoaji”

Kulingana na ripoti ya UNCTAD, shughuli za kijeshi za Israel zimeitupa Gaza “kutoka hali ya maendeleo duni hadi ile ya uharibifu kamili.” Umoja wa Mataifa unakadiria kwamba takriban dola bilioni 70 zitahitajika kujenga upya eneo la Palestina. “Hata katika hali yenye matumaini, ambapo ukuaji unafikia tarakimu mbili na misaada ya kigeni ikimiminika, itachukua miongo kadhaa kwa Gaza kurejesha ubora wa maisha yake ya kabla ya mwezi Oktoba 2023,” ripoti inabainisha.

UNCTAD inatoa wito wa utekelezaji wa “mpango kamili wa uokoaji” unaochanganya “msaada wa kimataifa ulioratibiwa, urejesho wa uhamisho wa fedha” kutoka Israel hadi Gaza “na hatua za kupunguza vikwazo vya biashara, usafiri, na uwekezaji.”

Shirika hili la Umoja wa Mataifa linatoa wito wa kuanzishwa, ndani ya mfumo huu, kwa mapato ya msingi ya jumla huko Gaza ili kutoa riziki kwa wakazi wote, katika mfumo wa mpango wa usaidizi wa pesa taslimu “unaoweza kufanywa upya na usio na masharti” unaolipwa kila mwezi. UNCTAD pia inabainisha kuwa katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, “vurugu, upanuzi wa haraka wa makazi, na vikwazo vya uhamaji wa wafanyakazi” vinasababisha kushuka kwa uchumi mbaya zaidi tangu shirika hilo lianze kufanya rekodi mwaka wa 1972.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *