Katika taarifa, shirika hilo la Umoja wa Mataifa linasema karibu watu milioni 35 kaskazini mwa Nigeria wanakadiriwa kuwa watakabiliwa na hali mbaya ya kutokuwa na usalama wa chakula kati ya Mei na septemba mwaka ujao wa 2026.

WFP linasema karibu watu 15,000 katika jimbo la Borno ambalo limekuwa kitovu cha mashambulizi ya kijihadi kwa kipindi cha miaka 16, wanakadiriwa kufikia kiwango cha hatari cha njaa.

Mashambulizi hayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 40,000 na kuwapelekea wengine karibu milioni 2 kaskazini mashariki mwa Nigeria kuachwa bila makao.

Wiki iliyopita tu, Nigeria ambayo ndiyo nchi yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, ilishuhudia utekaji nyara mkubwa wa watu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *