
Msemaji wa Jeshi la hilo kwa lugha ya Kiarabu, Avichay Adraee, amesema mashambulizi hayo ni katika kujibu kile wanachodai kuwa ni juhudi za Hezbollah kujaribu kuanzisha upya shughuli zake katika maeneo ambayo yamepigwa marufuku.
Kupitia ukurasa wake wa X, Adraee amesema wakazi wanaoishi karibu na majengo yanayotumiwa na Hezbollah wanapaswa kuyahama mara moja.
Katika chapisho hilo, ameambatanisha ramani zinazoonyesha vijiji vya Jbaa na Mahrouna, ambavyo vimetajwa moja kwa moja kwenye onyo la jeshi la Israel.