Mkutano huo utakuwa wa kutafuta suluhu kuhusiana na suala la kutolewa kwa fedha za Urusi zilizofungiwa, kuisaidia Ukraine.

Msemaji wa serikali ya Ujerumani amesema Merz ameahirisha safari yake ya kuelekea Norway ili asafiri kwenda Ubelgiji kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Bart de Wever na Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen.

Merz anasema viongozi wa Umoja wa Ulaya wanastahili kuwa na msimamo mmoja na wafikie makubaliano na Ubelgiji. Umoja wa Ulaya umependekeza kutumika kwa fedha hizo za Urusi zilizofungiwa huko Brussels kuisaidia Ukraine.

Waziri Mkuu wa Ubelgiji, De Wever lakini ameliambia bunge la nchi hiyo kuwa, Ubelgiji haitojitweka majukumu yatakayoitia nchi hiyo mashakani.

Fedha hizo za Urusi zinazosimamiwa na taasisi ya fedha ya Ubelgiji ya Euroclear, zinakadiriwa kuwa ni zaidi ya dola bilioni 215.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *