
Modi ameitaja ziara ya Putin kuwa kubwa na yenye kubeba umuhimu wa kihistoria kwa kuzingatia kwamba Putin aliitembelea India mara ya mwisho mwaka 2021. Putin ambaye yuko ziarani Urusiamesema ataendelea na “usafirishaji usiokatizwa” wa mafuta kwenda India, huku New Delhi ikikabiliwa na shinikizo kubwa la Marekani la kuacha kununua mafuta kutoka Moscow.
Putin amemwambia Modi kuwa Urusi ni muuzaji wa kuaminika wa mafuta, gesi, makaa ya mawe, na kila kitu kinachohitajika kwa ajili ya maendeleo ya nishati nchini India.
Ushirikiano huu wa India na Urusi unaonesha ni kwa jinsi gani sasa NewDelhi italazimika kuweka urari katika mahusiano yake baina ya Moscow na Marekani hasa kwa kuzingatia kwamba Marekani nimekuwa ikiishinikiza India kuutathmini upya uhusiano wake na Moscow.