
Costa amesema mjini Brussels kwamba ingawa ni kawaida kwamba Marekani na Ulaya hazina maono sawa kuhusu masuala mengi, lakini kitisho cha kuingiliwa siasa za ndani hakikubaliki.
Ametolea mfano wa tofauti ya maono kuhusu uhuru wa kujieleza kati ya Marekani na Ulaya na kusema hakuwezi kuwa na uhuru wa kujieleza ikiwa uhuru wa wananchi kupata taarifa utapindishwa ili kuwalinda watu wa tabaka la juu kama ilivyo nchini Marekani.