
Karibu watu 35,000 waishio kwenye maeneo ya mpaka nchini Thailand tayari wamehamishwa, hii ikiwa ni kulingana na vikosi vinavyohudumu kaskazinimashariki, kaskazini na kusini mwa Thailand.
Waziri wa habari wa Cambodia Neth Pheaktra ameiambia AFP kwamba karibu raia wanne wa Cambodia waliuawa kwa mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa Thailand hii leo katika maeneeo ya mpakani ya Preah Vihear na Oddar Meanchey.
Karibu raia wengine 10 walijeruhiwa.
Mgogoro huo umechochewa na tofauti za muda mrefu kuhusu mipaka iliyochorwa enzi ya ukoloni wa Ufaransa katika eneo hilo, ambapo pande zote mbili zinadai umiliki wa mahekalu ya kale yaliyopo mpakani.