Mawakili wa rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro, aliyehukumiwa kifungo cha miaka 27 jela kwa jaribio la mapinduzi, wameiomba Mahakama Kuu kuidhinisha mteja wao kulazwa hospitalini kwa ajili ya upasuaji, kulingana na hati zilizopatikana siku ya Jumanne, Desemba 9, 2025, na shirika la Agence France-Presse (AFP).

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Nyaraka zote mpya zilizowasilishwa hivi karibuni (…) zinaelezea kuzorota kwa afya” ya kiongozi huyo wa zamani wa mrengo wa kulia mwenye umri wa miaka 70, kulingana na hati, zinazoomba “kulazwa hospitalini mara moja.”

Kulishuhudiwa pia vurugu katika Bunge la Brazil siku ya Jumanne wakati wabunge walipokuwa wakiupigia kura muswada ambao unaweza kupunguza  kifungo cha Bolsonaro  mwenye umri wa miaka 70 na ambaye aligunduliwa na saratani mwezi Septemba.

Kiongozi huyo wa zamani wa Brazil kutoka chama cha siasa za mrengo wa kulia alianza kutumikia kifungo chake mwezi Novemba mwaka huu, baada ya kupatikana na hatia ya kuandaa mpango wa kumzuia Rais wa sasa Luiz Inacio Lula da Silva kuchukua madaraka baada ya uchaguzi wa mwaka 2022, kitendo kilichochukuliwa kama jaribio la mapinduzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *