
Serengeti. Shirika la Grumeti Fund limewapeleka wanafunzi wawili nchini Taiwan ili kujifunza namna bora ya kukabiliana na mbadilikao ya tabia nchi sambamba na njia bora na ya kisasa ya upandaji miti.
Wanafunzi hao ni Flora Gesimba wa Shule ya Sekondari Natta na Cosmas Kitena wa Shule ya Sekondari Issenye ambao wamepata ufadhili wa shirika hilo kupitia idara yake ya maendeleo ya jamii ambapo wakiwa nchini Taiwan pia watapata fursa ya kutembelea vituo vya utamaduni, mazingira sambamba na kukutana na wabobezi katika masuala ya mazingira ili kujifunza kuhusu utunzaji ea mazingira endelevu.
Wanafunzi hao wanaotarajiwa kukaa nchini Taiwan kwa siku kumi ambapo pia watapata fursa ya kujifunza kuhusu utunzaji wa maliasili, mazingira pamoja na vyanzo vya maji na kubadilisha taka kuwa fursa kwenye maeneo yao.
Kwa mujibu wa Mkuu wa kituo cha Elimu ya Mazingira Grumeti Fund, Laurian Lamatus amesema ziara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa programu ya elimu ya mazingira ambayo imekuwa ikifanywa na shirika hilo kwa muda mrefu ili kujenga kizazi chenye uelewa juu ya umuhimu wa uhifadhi wa mazingira na maliasili.
Amesema kituo hicho kinapokea na kufundisha vijana zaidi ya 500 kila mwaka kutoka katika shule 16 zilizopo pembozoni mwa hifadhi ya Taifa ya Serengeti katika wilaya za Bunda na Serengeti mkoani Mara.
“Ili kuwapata hawa wanafunzi wawili,tulifanya mashindano ya kuandika insha pamoja na shughuli zingine zinazohusu mazingira,mashindano ambayo yalishirikisha wanafunzi zaidi ya 30 kutoka shule 16 katika wilaya za Bunda na Serengeti na washindi wakapatikana,” amesema
Lamatus amesema kupitia programu hiyo wamekuwa na ushirikiano na wanafunzi wengine kutoka nchini Taiwan kwa lengo la kubadilishana uzoefu kutoka katika nchi hiyo.
Amesema ushirikiano huo umekuwepo kutokana na kuwepo kwa wanafunzi katika nchi hiyo ya Taiwan ambao pia wanaishi katika maeneo mapori ya akiba na kwamba hivi sasa wanafunzi hao wanakwenda kujifunza kwa vitendo.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Grumeti,Frida Mollel amewapongeza wazazi kwa kuwa karibu na watoto wao katika kuhakikisha wanatimiza ndoto zao na kutambua umhimu wa kujifunza kuhusu mazingira.
Amewataka wanafunzi hao kutumia kutumia safari hiyo kama chachu ya mabadiliko chanya ya kifkira juu ya utunzaji wa mazingira na kuwataka kuwa mabolozi wazuri kampuni ya Grumeti fund.
“Ninawapongeza wanafunzi na wazazi kwa kupata nafasi hii adhimu niwaombe mkatumie fursa hii kubadili fikra zenu juu ya utunzaji wa mazingira, kumbukeni mmebeba sura ya Grumeti huko muendako basi hakikisha mnakuwa mabalozi wazuri” amesema
Wazazi na wanafunzi hao ambao wamepata fursa hiyo wamelipongeza shirika hilo huku wakisema watoto wao wamepata mwanzo mpya wakutambua fursa na kusema kuwa wanaamini watakuwa mabalozi wazuri wa mazingira nchini. Hariri habari hii kwa style ya Mwananchi