MSANII wa muziki anayefahamika kwa jina la Haroun Rashid maarufu kama Inspekta Haroun Babu ameweka wazi matarajio yake ya kuendelea kufanya kazi na wasanii mbalimbali wanaofanya vizuri katika muziki wa Bongo Fleva kwa sasa.
Akizungumza na HabariLEO, Inspector Haroun Babu alisema tayari ana miradi kadhaa ya muziki inayoendelea, huku mingine ikiwa imekamilika. Amesema miongoni mwa wasanii anaotarajia kufanya nao kazi ni Country Boy, G Nako na Jux.
Aidha, msanii huyo alizungumzia tetesi zinazodai kuhusishwa kwake na kampeni mbalimbali, ikiwemo zinazohusu masuala ya muziki na siasa. Ameweka wazi kwamba hahusiki na kampeni yoyote na hana uhusiano wowote na chama chochote cha siasa. “Sijihusishi na siasa kwa namna yoyote ile, sina chama wala kampeni yoyote,” alisema Inspector Haroun Babu.
Katika hatua nyingine, amekanusha madai kuwa anajiandaa kuacha muziki, akibainisha kuwa bado ana hamu kubwa na anaiona tasnia ikimhitaji. “Sina mipango ya kuacha muziki kwa sababu bado naona muziki unaniitaji,” alisema. SOMA: Stara: Sitaacha kuimba nyimbo za zamani
