Lakini badala yake anasema iko tayari kuchukua jukumu la kushiriki katika miundo iliyomo kwenye azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kama vile baraza la amani, ingawa bado pia bado haijapokea mwaliko rasmi wa kushiriki katika baraza hilo. Aidha Wadephul anataka kuanza haraka kwa Awamu ya pili ya mpango wa amani. Awamu ya pili ijayo ya mpango wa amani wa vipengele 20 wa Rais wa Marekani Donald Trump inataka kuvunjwa kwa nguvu ya kivita ya kundi la wapiganaji wa Kipalestina Hamas na kuanzishwa kwa kikosi hicho cha ulinzi wa amani cha kimataifa ISF.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *