#HABARI: Licha ya jitihada za Serikali kuondoa ada katika elimu ya msingi na sekondari, bado kumejitokeza changamoto ya baadhi ya wazazi kutowapeleka watoto wao shule kwa wakati.

Kasumba hiyo inatokana na wazazi kudai kukosa uwezo wa kununua sare za shule, jambo ambalo limekuwa likikwamisha malengo ya elimu kwa watoto wengi nchini.

Ili kutatua changamoto hiyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Diwani wa Kata ya Utengule Usangu, Ismail Matipa, amechukua hatua ya kuwashonea sare za shule wanafunzi zaidi ya 400.

Wanafunzi hao ni wale waliochelewa kuripoti au walio na mahitaji ambao wanatarajia kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za kata hiyo.

Akizungumzia hatua hiyo, Mkuu wa Shule Msaidizi wa shule ya kata ya Utengule Usangu, Mwalimu Hagachi Julius, amebainisha kuwa msaada huo utaleta tija kubwa. Ameeleza kuwa awali shule zilikuwa zikikabiliana na mahudhurio hafifu wakati wa kufungua shule, lakini kupatikana kwa sare hizo kutahakikisha wanafunzi wote wanaripoti kwa wakati na kuanza masomo bila kikwazo.

Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *