
Mvutano wa kidiplomasia katika Pembe ya Afrika unaendelea kufuatia tangazo la Israel la kuitambua uhuru wa Somaliland, eneo linalotaka kujitenga kaskazini mwa Somalia. Rais wa Somalia anaishutumu serikali ya Israel kwa kuweka masharti kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuwahamisha Wapalestina na kuanzishwa kwa kambi ya kijeshi—shutuma ambazo zimekanushwa na mamlaka ya Somaliland.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na rais wa Somalia, tangazo la Israel la kutambua uhuru wa Somaliland kulitokana na masharti matatu: kuwahamisha Wapalestina katika eneo linalotaka kujitenga la Somalia, kuanzishwa kwa kambi ya kijeshi katika Ghuba ya Aden, na kufuata Mkataba wa Abraham ili kufufua uhusiano na Israel.
Madai haya yamekanushwa haraka na Wizara ya Mambo ya Nje ya Somaliland, ambayo imeyaita “shutuma za uwongo.” Katika taarifa rasmi, Mohamed Bihi Yonis amekana kuwepo kwa mipango ya kuwahamisha Wapalestina na kufutilia mbali wazo la kituo kambi ya kijeshi ya Israel katika eneo lake.
Somaliland ni eneo linalojitegemea la Somalia ambalo lilitangaza uhuru wake mwaka wa 1991. Wiki iliyopita, Israel ikawa taifa la kwanza kulitambua kama “taifa huru,” na kuimarisha zaidi uhusiano wake na mshirika wake muhimu.
Kwa Israeli, Somaliland inashikilia nafasi ya kimkakati kwenye Mlango-Bab-el-Mandeb, karibu na waasi wa Houthi huko Yemen, ambao wanaungwa mkono na Iran na wameanzisha mashambulizi mengi dhidi ya Israel tangu kuanza kwa vita vya Gaza.