
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwenye mtandao wake wa Truth Social siku ya Ijumaa kwamba “ikiwa Iran itawapiga risasi waandamanaji wa amani na kuwaua kwa nkiholela, kama ilivyo kawaida yake, Marekani itawasaidia”.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Tuko tayari, tumejihami, na tumejiandaa kuingilia kati,” ameandika, huku makabiliano kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama yakisababisha vifo vya watu sita nchini Iran siku ya Alhamisi, vifo vya kwanza tangu kuanza kwa maandamano dhidi ya kupanda kwa gharama ya maisha nchini humo.
Mapema siku hiyo, polisi pia walitumia silaha za moto katika jiji la magharibi la Lordegan. Kulingana na shirika la habari la Fars, waandamanaji “walianza kurusha mawe kwenye majengo ya utawala, ikiwa ni pamoja na makao makuu ya mkoa, msikiti, ukumbi wa jiji, na benki.” Shirika hilo linaripoti kwamba watu wawili waliuawa hapo, wakionekana kuwa raia, kulingana na shirikala habari la AFP.
Soma piaIran: harakati za maandamano zinaendelea na zimejikita katika miji ya majimbo
Video nyingi pia zimeshirikiwa zikionyesha makundi ya waandamanaji katika miji mingine ishirini ya mkoa, anaripoti mwandishi wetu huko Tehran, Siavosh Ghazi. Huko pia, polisi walitumia gesi ya machozi na silaha za moto.
Kinyume na matarajio, jiji la Tehran, ambalo ndilo mwanzo wa harakati hiyo siku ya Jumapili, Desemba 28, liliedelea kuwa shwari. Hata hivyo, shirika la habari la Tasnim limeripoti kwamba watu 30 walikamatwa katika mji mkuu kwa “kuvuruga utulivu wa umma.” Vyombo vya habari vya ndani vinakadiria kwamba jumla ya idadi ya waliokamatwa ni karibu 100.
Jaribio la kupunguza mvutano
Siku ya Ijumaa, Januari 2, na Jumamosi, Januari 3, zimetangazwa kuwa sikukuu za umma. Mamlaka pia imetangaza kwamba visomo katika vyuo vikuu vyote katika mji mkuu yangefanyika kwa nia ya video hadi Januari 9 ili kuzuia mikusanyiko.
Mgomo wa wafanyabiashara katika soko la mji mkuu, kufuatia kuanguka kwa rial (sarafu ya Iran)—ambayo imeshuka thamani kwa karibu theluthi moja dhidi ya dola katika kipindi cha mwaka mmoja—uligeuka kuwa wa kisiasa haraka kwa kuhusika kwa wanafunzi, na kisha kuenea hadi miji ya majimbo ambapo mapigano mengi yalitokea.