Utawala wa kijeshi nchini Myanmar umetangaza leo Jumapili, Januari 4, kwamba utawaachilia huru zaidi ya wafungwa 6,000 kama sehemu ya msamaha wa kila mwaka kwa kuadhimisha sikukuu ya kitaifa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Kaimu Rais wa Muungano wa Jamhuri ya Myanmar amewasamehe wafungwa 6,134, wanaume kwa wanawake, waliokuwa wakitumikia vifungo vyao katika magereza, vituo vya kizuizini, na kambini,” Baraza la Kitaifa la Ulinzi na Usalama la utawala wa kijeshi limesema katika taarifa.

Wafungwa hamsini na wawili wa kigeni pia wataachiliwa huru na kufukuzwa nchini, kulingana na taarifa tofauti. Utawala wa kijeshi nchini Myanmar umewakamata maelfu ya waandamanaji na wanaharakati tangu mapinduzi yake ya Februari 2021, ambayo yaliitumbukiza nchi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Habari zaidi zinakujia…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *