Hali bado ni tete kusini mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambayo imekumbwa na mapigano makali kati ya jeshi na wanamgambo wa AAKG tangu wiki iliyopita.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tangu wiki iliyopita, mkoa wa Haut-Mbomou kusini mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati umekumbwa na mapigano makali kati ya vikosi vya serikali na wanamgambo wa Azandé Ani Kpi Gbé (AAKG), kundi la kujilinda kutoka jamii ya Zande ambalo limeasi dhidi ya serikali huko Bangui. Mji wa Zémio ulilengwa tena katika shambulio usiku wa Jumapili, Januari 4, kuamkia Jumatatu, Januari 5.

Kwenye picha zilizorushwa hewani kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha kanisa la mji huo limebadilishwa kuwa kambi halisi ya watu waliokimbia makazi yao. Misheni ya Wakatoliki, kama ilivyotokea hapo awali, imefungua milango yake kwa kila mtu, anaelezea Askofu Aurelio Gazzera wa Bangassou.

Watu elfu mbili wameripotiwa kupata hifadhi katika, kambi hiyo, na pia hospitalini, kulingana na chanzo cha kidini, huku wengine wakikimbia na kuvuka mpaka na kuingia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) baada ya wikendi ya vurugu katika vitongoji kadhaa. Askofu Gazzera anaelezea kukimbia kwa watu hawa kama tatizo, akisema kwamba watu wengi tayari wamevuka mto na kuingia Kongo jirani, au wataendelea kufanya hivyo.

Hakuna nafasi nyingi katika misheni, lakini kama ilivyotokea mara nyingi hapo awali, wanafungua milango yao kwa kila mtu. Tatizo kubwa ni kwamba watu wengi tayari wamevuka mto na kuingia Kongo jirani, au wataendelea kufanya hivyo. Tatizo lingine kubwa ni hali ya kiafya kwa sababu hospitali ilishambuliwa. Kwa vyovyote vile, rasilimali tayari ni chache, na hili ni suala kubwa. Na wasiwasi mwingine, mkubwa zaidi ni kwamba eneo hilo limeteketea kwa moto kutoka Bambouti, kwenye mpaka na Sudan Kusini, hadi Zemio. Ni takriban kilomita 350 hadi 400, na ni eneo lote linalowaka moto.

Askofu Aurelio Gazzera wa Bangassou ameonya kuhusu hali huko Zemio.

Ingawa utulivu dhaifu umerejea na MINUSCA inafanya doria, hakuna takwimu rasmi zilizopatikana bado. Vyanzo vinaripoti vifo kadhaa na majeruhi wengi miongoni mwa vikosi vya serikali na washirika wao wa Urusi, ambao wanamgambo wa AAKG wanataka waondoke, pamoja na kuachiliwa kwa viongozi wao wanaozuiliwa.

Kuhusu mkuu wa mkoa wa Bambouti na polisi ambaye alitekwa nyara pamoja naye Jumapili, Desemba 28, siku ya uchaguzi mkuu, bado hakuna habari yoyote kuhusu wapi waliko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *