Dar es Salaam. Konde kachakazwa na huba la ‘Da Kei’ wa Obey. Konde hasikii la muadhini wala mnadi swala. ‘Da Kei’ naye ni kama vile kashindwa kubana jumla jumla. Wapendana haswa wawili hawa.

‘Muhuni’ wa Tandahimba, aliye na muhuri wa makazi ya korido za mitaa ya Msimbazi na Uhuru. Yes! Wakati anajitafuta aliweka kambi mitaani kabla msela wa Tandale kumuinua. 

Kajala alikuwa staa Konde akiwa mtoto wa mtaani. Kajala wa Obey Polisi, Konde toto la Tandahimba uswekeni. Leo hii ana kila kitu ambacho kijana anapaswa kuwa nacho.

Kuna vitu ndani ya Kajala vigeni kwa Konde. Na kuna vitu ndani ya Konde Boy vigeni kwa Kajala. Yes, ndo maana wanapeana mgongo na kurudiana kama ruti za mabasi ya mwendokasi.

Konde Boy na Kajala ni kama JB Mpiana na Amida. Huyu Amida ndiye mwanamke aliyeurndesha atakavyo moyo wa JB Mpiana,  Bosi la Wenge Bcbg. Jibe kamwe hajawahi kusitisha pendo kwa hii pisi.

JB Mpiana na Amida Shatur, walikaa katika ndoa toka 1997 hadi 2003. Walifanikiwa kupata watoto watatu, na 2001 uvumi ulianza kuvuma kwamba wawili hawa wametengana.

Walijitahidi kuficha siri, mwisho wa siku zikavuja. Baada ya JB  kuchukua uamuzi wa kuhama nyumbani kwake. Akimuachia mkewe makazi yao na kuhamia mtaa mwingine. 

Kumbe mkewe ana uhusiano na tajiri Didi Kinuani. Ambaye pia ni rafiki mkubwa wa JB Mpiana. Ni kwamba tajiri aliamua kutafuna mali ya mshikaji wake na kuweka kambi jumla jumla. 

JB akajibebea pisi mpya iitwayo Bebe Mulumba akaweka ndani na kuoa. Pisi ya maana kweli. Asili ya JB ni kabila la Waluba, ambalo kwao ni mwiko kabisa kumrudia mke aliyetoka nje ya ndoa.  

Kwa mshangao wa wengi pamoja na familia, JB akatoa talaka kwa Bebe Mulumba. Kwa mshangao wa wengi, JB akarudi ‘eksi’ wake Amida Shatur. Hapo bishoo wa Kinshasa hasikii la mtu.

Mpaka leo JB Mpiana na Amida wanaendelea na ndoa yao. Kwa kifupi jamaa alirudi tapishi lake na kulipenda mara mbili zaidi. Mapenzi bado yapo kwenye huu ulimwengu.

Konde naye alijiweka kwa Posh Queen baada Kajala kuzingua. Watu wakijua ni jibu kwa Kajala. Yupo wapi Posh? Konde karudi kwa Kajala na haambiwi kitu. Na Kajala haambiwi kitu kwa Konde Boy.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *