
Dar es Salaam. Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel nchini, imesema uwekezaji mkubwa iliyoufanya katika miundombinu ya mawasiliano, umesaidia kufikia wateja 16.5milioni ndani ya kipindi cha miaka 10.
Idadi hiyo ya wateja ni kuanzia mwaka 2015 ilipoanzishwa kampuni hiyo hapa nchini hadi Septemba 2025.
Kutokana na ukuaji huo, Kampuni hiyo, imetoa gari aina ya Subaru Forester XT kwa mshindi wa kampeni ya kutimiza miaka 10 nchini ya utoaji wa huduma za mawasiliano ya Halotel nchini.
Mshindi wa gari hilo, Magdalena Nkuba kutoka Simiyu, ametangazwa leo Jumanne, Januari 6, 2026 katika droo kubwa iliyochezeshwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Halotel, Roxana Kadio amesema hayo, baada ya kuchezeshwa kwa droo ya kumpata mshindi wa gari kupitia kampeni hiyo.
Amesema katika kuunganisha wananchi, kampuni hiyo itaendelea kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma ya mawasiliano yenye ubora, gharama nafuu na mahali popote.
“Mafanikio haya yametokana na uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya mawasiliano, na ndiyo maana tunahudumia mamilioni ya wateja kwa kuwaunganisha kutoka vijijini hadi mijini, hasa maeneo ambayo hapo awali hayakuwa na mtandao,” alisema Salum na kuongeza na kuongeza
Amesema kampuni hiyo inaendelea kuimarisha huduma zake kwa kujali wateja, kutoa huduma bora za mawasiliano, kuboresha maisha ya watumiaji wake, hivyo jamii itumie huduma hiyo kwani ni rahisi.
“Oktoba 2025 tulianzisha kampeni ya kufikisha miaka 10 ya utoaji wa huduma za mawasiliano hapa nchini na kampeni hii iliendeshwa kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Oktoba” Alisema Kadio
Amesema promosheni ya wateja kuweza kujishindia zawadi ya gari kupitia miamala ya Halopesa waliyokuwa wanatumia kuanzia Sh2000 na kuendelea.
Hata hivyo, kabla ya kutoa zawadi hiyo kubwa ya gari, ilitanguliwa na droo nyingine kwa ajili ya kupata washindi w fedha taslimu kuanzia Sh2milioni.
“Leo katika droo ya kampeni hii, mteja wetu kutoka mkoani Simiyu Magdalena Nkuba amefanikiwa kushinda gari aina ya Subaru XT mpya, hivyo atapewa utaratibu wa namna ya kupokea zawadi ya gari” alisema Kadio.
Elibariki Sengasenga ni Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania, anasema bodi imefuata taratibu zote ili kuhakikisha mshindi anapatikana kihalali.
Ameshinda kwa haki na kila mtu anashuhudia.
“Wito wangu kwa kampuni zingine, zifuate utaratibu kama inavyotakiwa kwa kupata kibali kutoka bodi ya Michezo ya kubahatisha ili watu wanaamini” alisema Sengasenga.