Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi ameanza hivi leo ziara yake ya kila mwaka katika mataifa ya bara la Afrika, akilenga hasa eneo muhimu la kimkakati la Mashariki mwa Afrika.

Ziara ya mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu wa China itamfikisha katika nchi za Ethiopia, Somalia Tanzania na Lesotho, wakati nchi yake ikitafuta kuimarisha ushawishi wake katika bara hilo.

China yaipa Afrika mkopo wa dola bilioni 20

Ziara ya Wang nchini Somalia ambayo ni ya kwanza kuwahi kufanywa na waziri wa mambo ya nje wa China tangu miaka ya 1980, huenda ikawa ni nafasi ya kuipatia sauti Mogadishu kwenye suala la diplomasia baada ya Israel mwezi uliopita kuwa nchi ya kwanza duniani kuitambuwa rasmi Jamhuri ya Somaliland iliyojitenga na Somalia baada ya kujitangazia uhuru wake mwaka 1991.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *