Cyprus imechukua rasmi nafasi ya kupokezana ya mwenyekiti  wa Umoja wa Ulaya leo Jumatano, ikianza muhula wake kwa mkutano uliohudhuriwa na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy, Rais wa halmashauri ya Ulaya Ursula von der Leyen, pamoja na Rais wa Baraza la Ulaya Antonio Costa.

Washirika wa Ukraine wakutana Paris, hatma ya usalama bado shakani

Washauri wa usalama wa EU wakutana Kiev kwa mazungumzoBaadaye leo, hafla maalum itafanyika mjini Nicosia kuashiria mwanzo wa muhula wa miezi sita wa Cyprus, ikiwajumuisha pia viongozi kutoka Mashariki ya Kati, akiwemo Rais wa Lebanon Joseph Aoun. Hatua hiyo inaonesha dhamira ya Cyprus kuwa daraja kati ya Ulaya na eneo hilo.

Rais Zelenskiy alipokelewa  na Rais wa Cyprus Nikos Christodoulides, akieleza matumaini kuwa uwenyekiti wa Cyprus utaisaidia nchi yake kupiga hatua kuelekea kupata uanachama wa Umoja wa Ulaya. Mzozo wa Ukraine

Ziara ya Zelenskiy pia imelenga  kujadili yaliyojitokeza kwenye mkutano wa Paris uliofanyika jana Jumanne, ambako Marekani iliunga mkono muungano mpana wa washirika wa Ukraine kutoa hakikisho la kiusalama iwapo usitishaji vita utafikiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *