#HABARI: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, amesema Serikali inatambua umuhimu wa kuwepo kwa jukwaa rasmi litakalowawezesha vijana kutoa maoni, mawazo na ushauri wao kuhusu masuala yanayowahusu moja kwa moja.

Akizungumza leo Januari 10, 2026 wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Vijana (Vijana Platform) uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, Nanauka amesema jukwaa hilo ni nafasi mpya ya kimkakati itakayowawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika mijadala ya maendeleo yao wenyewe.

Alisema kupitia Vijana Platform vijana watapata fursa ya kusikika, kushiriki na kuchangia moja kwa moja katika kujadili masuala ya ustawi wao, maendeleo ya kijamii na kiuchumi pamoja na mustakabali wa taifa kwa ujumla.

“Kupitia Vijana Platform, vijana wanapewa nafasi ya kusikika, kushiriki na kuchangia moja kwa moja katika kujadili masuala ya ustawi wao, maendeleo ya kijamii na kiuchumi pamoja na mustakabali wao,” amesema Nanauka.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *