
Rais wa Marekani Donald Trump amesema siku yaJumapili, Januari 11, kwamba viongozi wa Iran wako tayari kwa “majadiliano” baada ya vitisho vyake vya kuchukua hatua za kijeshi, huku Jamhuri ya Kiislamu ikikabiliana na maandamano makubwa ya kupinga serikali.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Viongozi wa Iran walitupigia simu” Jumamosi, Trump amewaambia waandishi wa habari ndani ya ndege ya Air Force One, akiongeza kwamba “mkutano unaandaliwa… Wako tayari kwa kujadili nasi.”
Hata hivyo, rais wa Marekani ameonya kwamba “tunaweza kulazimika kuchukua hatua kabla ya mkutano.”
Wakati huo huo shirika la kutetea haki za binadamu la Iran lenye makao yake nchini Norway limesema mamlaka za Iran zimefanya mauaji ya halaiki.
“Maafisa wa mamlaka za Iran wamefanya mauaji ya halaiki katika kukandamiza maandamano makubwa zaidi dhidi ya jamhuri ya Kiislamu kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka mingi”, shirika hilo limesema.
Kwa mujibu wa kundi la haki za binadamu lenye makao yake makuu Marekani, takriban waandamanaji 490 na wanajeshi 48 wameuawa.
Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kufanya mkutano na maafisa wake wakuu kesho Jumanne, kujadili njia za kujibu maandamano nchini Iran.