Rwanda imetangaza siku ya Jumatatu, Januari 12, katika mahojiano na Jeune Afrique, kwamba Kigali itawasilisha barua ya kugombea kwa Louise Mushikiwabo kwa muhula wa tatu kama mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nchi zinazozungumza Kifaransa (OIF). Tangazo hili linakuja miezi kumi kabla ya mkutano ujao wa kilele wa Nci zinazungumza Kifaransa, uliopangwa kufanyika mwezi Novemba huko Phnom Penh, Cambodia.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Kigali, Lucie Mouillaud

Kwa Waziri wa Mambo ya Nje Olivier Nduhungirehe, rekodi ya Louise Mushikiwabo “inayotambulika na kusifiwa sana” akiwa mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nchi zinazozungumza Kifaransa inahalalisha uungaji mkono wa serikali kwa mgombea wake.

Alipoulizwa na Jeune Afrique kuhusu uwezekano wa Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kupinga tangazo hili, mkuu wa diplomasia ya Kigali amesema kwamba kila nchi mwanachama ina haki ya kuwasilisha maombi yake.

Baada ya miaka saba akiwa katika uongozi wa OIF (Shirika la Kimataifa la La Francophonie), muhula wa sasa wa Louise Mushikiwabo unamalizika mwishoni mwa mwaka. Novemba mwaka jana, kando ya mkutano wa mawaziri wa shirika hilo, Waziri hyuo wa zamani wa Mambo ya Nje wa Rwanda alisema kwamba nchi kadhaa tayari zilimuona, zikimwomba agombee tena nafasi ya Katibu Mkuu wa La Francophonie. Kipindi cha kuwasilisha barua za kugombea kwenye nafasi hiyo kinaisha mwezi Aprili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *