
Kwa mujibu wa jeshi la anga la Ukraine, vikosi vya Urusi pia vimefanya mashambulizi katika miji ya Kyiv, Odessa na miji mingine usiku kucha kwa kutumia droni na makombora ya masafa marefu.
Katika mji mkuu Kyiv, mamlaka imelazimika kuzima umeme kwa dharura ili kuzuia uharibifu zaidi kufuatia mashambulizi hayo ya Urusi.
Wakati huohuo, mamilioni ya watu katika miji mikubwa ya Ukraine wanakabiliwa na baridi kali bila umeme na maji kutokana na uharibifu wa miundombinu ya nishati.
Ukraine nayo imefanya mashambulizi ya droni ndani ya Urusi usiku wa kuamkia leo. Mamlaka katika mkoa wa Rostov zimeripoti kuwa kiwanda katika mji wa Taganrog kimeshambuliwa.
