Iran: Marekani yatafuta ‘kisingizio cha kuingilia kijeshi’Iran: Marekani yatafuta ‘kisingizio cha kuingilia kijeshi’

Serikali ya Iran imeishutumu Marekani kwa kutafuta kutengeneza kisingizio cha kuingilia kati kijeshi, baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutishia “hatua kali” kuhusu ukandamizaji mbaya dhidi ya maandamano makubwa.

Ujumbe wa Iran katika Umoja wa Mataifa ulichapisha taarifa kwenye mtandao wa X, ukisema ndoto na sera za Marekani kuelekea Iran zimejikita katika mabadiliko ya utawala, huku vikwazo, vitisho, machafuko yaliyoandaliwa, na vurugu yakitumika kama njia ya kutengeneza kisingizio cha kuingilia kati kijeshi.

Ujumbe huo umeapa kwamba mchezo wa Marekani utashindwa tena. Iran imemtuhumu rais Trump Jumanne kwa kuchochea uvunjifu wa uthabiti wa kisiasa, kuchochea vurugu, na kutishia uhuru wa nchi na usalama wa taifa.

Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa Amir Saeid Iravani aliandika katika barua yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa akisema “Marekani na utawala wa Israeli zinabeba dhamana ya kisheria ya moja kwa moja na isiyopingika kwa vifo vya raia wasio na hatia, hasa miongoni mwa vijana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *