
Wenyeji wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika nchini ya Morocco, wamefanikiwa kuingia hatua ya fainali baada ya kufanikiwa kuwaondoa Nigeria, na sasa watacheza fainali na mabingwa wa mwaka 2021, Senegal.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Morocco walifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya ushindi wa Penati 4 kwa 2 dhidi ya Nigeria baada ya dakika tisini timu hizo kushindwa kufungana katika mchezo uliofanyika mjini Rabat.
Ushindi wa Morocco unawaweka vijana hao wa Mfalme Mohamed wa 6 katika njia ya uwezekano wa kutwaa taji lake la pili la michuano hiyo baada ya lile ililochukua mwaka 1976.
Kwa upande wake Senegal ambao ni mabingwa wa taji hilo mwaka 2021, walitinga hatua ya fainali baada ya kupata ushindi wa bao 1 – 0 dhidi ya Misir walilolipata katika dakika za lala salama likifungwa na mshambuliaji wake, Sadio Mane.
Ushindi wa Senegal, ulizima rasmi matumaini ya mshambuliaji wa Misri Mohammed Salah, ambaye licha ya timu yake kushikiliza rekodi ya kushinda taji hilo mara 6, yeye tangu ajiunge na timu ya taifa hajawahi kufanikiwa.
Mechi ya fainali sasa itachezwa Jumapili ya tarehe 18 saa nne usiku, huku Nigeria wao wakitarajiwa kucheza na Misri siku ya Jumamosi kuwania nafasi ya mshindi wa tatu.
