Mazungumzo kuhusu mzozo wa Sudan yameanza tena mjini CairoMazungumzo kuhusu mzozo wa Sudan yameanza tena mjini Cairo

Mazungumzo ya kujaribu kupata Suluhu ya mzozo wa Sudan yameanza mjini Cairo, ambapo waziri wa mambo ya nje wa Misri, Badr Abdelatty, amesema nchi yake haitasita kuchukua hatua stahiki kulinda umoja wa taifa hilo la pembe ya Afrika, wakati huu vita nchini humo ikiingia mwaka wanne.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo haya yanayolenga kusaidia upatikanaji wa mwafaka nchini Sudan, na yamerejelewa wakati huu makabiliano kati ya jeshi la serikali na wapiganaji wa RSF yakishika kasi.

Wapiganaji wa RSF wamekuwa wakipmbana na jeshi la serikali tangu mwezi Aprili mwaka wa 2023, huku juhudi za awali za kusitisha mapiganao zikionekana kugonga mwamba.

Massad Boulos, mshauri wa Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu masuala ya nchi za kiarabu na Afrika Pamoja na mjumbe wa katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Ramtane Lamamra wamehudhuria majadiliano hayo.

Mzozo wa Sudan umetajwa na mashirika ya kibinadamu Pamoja na umoja wa Mataofa, kuwa moja kati ya mizozo mikubwa zaidi ya kibinadamu duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *