Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wimbi linaloendelea la kamata kamata halilengi tu wanasiasa au maafisa wa usalama. Pia linawalenga ndugu wa Corneille Nangaa, mwenyekiti wa zamani wa Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi na mratibu wa sasa wa AFC/M23.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wanafamilia wake kadhaa kwa sasa wako uhamishoni au wamezuiliwa. Kesi ya hivi karibuni inamhusu Didier Ilaani Nangaa, aliyekamatwa na kuzuiliwa kwa siku kumi na tatu katika kituo cha Idara ya ujasusi katika mkoa wa Haut-Uele, kulingana na duru za kuaminika.

Kulingana na taarifa zetu, Didier Ilaani Nangaa alihojiwa mara kadhaa na idara za usalama. Wakati huu, anahusishwa na mzozo wa madini—suala linalojirudia katika kesi zinazomhusu Corneille Nangaa—zinazohusiana na makubaliano yauchimbaji wa dhahabu.

Kulingana na taarifa zetu, mamlaka zimekuwa zikichunguza mitandao inayowezekana ya ufadhili wa AFC/M23 kwa miaka miwili. Pia wanatafuta hifadhi za silaha zinazowezekana katika eneo la Wamba mkoani Haut-Uélé. Utafutaji wa kina tayari ulifanyika katika eneo hili mwaka wa 2024. Mwaka huo huo idazra za usalama walifanya msako katika nyumba ya baba yake Corneille Nangaa mwenye umri wa miaka 86.

Wanafamilia wanne wahukumiwa kifo

Leo, wanafamilia wanne wa Corneille Nangaa pia wamehukumiwa kifo. Miongoni mwao ni kaka yake, Baseane Nangaa Putters, ambaye kwa sasa amefungwa katika gereza la kijeshi la Ndolo. Mke wa Corneille Nangaa, Yvette Lubanda, yuko uhamishoni, kama vile shemeji yake, Fabrice Lubala. Ndani ya familia hiyo pana, angalau wajukuu na binamu kadhaa wanaripotiwa kushikiliwa katika vituo mbalimbali, kulingana na hati ya ndani tuliyoipata.

Hatimaye, kulingana na vyanzo vyetu, wanafamilia wengine kadhaa waliondoka katika ardhi ya Kongo katika miaka miwili iliyopita na sasa wako katika nchi zinazopakana na DRC, na pia kwingineko barani Afrika na Amerika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *