[ad_1]

s

Bila shaka wanahistoria wanaendelea kukusanya takwimu za namna uchaguzi mkuu wa Tanzania 2025 huu utakumbukwa miaka ya mbeleni. Lakini hadi kufikia sasa, tayari kipo ambacho bila shaka hakitaachwa kutajwa.

Kwamba wakati wagombea wa chama cha tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiendelea kuchanja mbuga kujinasibu kwa kile walichowafanyia Watanzania na kuwaahidi watakachowafanyia miaka mingine mitano ijayo, washindani tunaoweza walau kuwaita wa kiwango chao wanazunguka katika valanda za mahakama – mmoja akipigania kurejeshwa kwenye ulingo wa mapambano mwingine akipambana kupangua kesi ya uhaini, ambayo akikutwa na hatia itamgaharimu uhai wake.

Kwa miaka thelathini iliyopita, awamu sita za uchaguzi mkuu, nyakati kama hizi hali ilikuwa tofauti. Hata kwa uchaguzi wa kwanza kabisa baada ya kurejeshwa mfumo wa vyama vingi vya siasa, mgombea wa chama tawala hakuteleza mithili ya kushuka mlima Kitonga mkoani Iringa, bali alipambana na mshindani aliyemtoa jasho kweli kweli.

Mkapa vs Mrema

S

Chanzo cha picha, HL

Maelezo ya picha, Benjamin Mkapa akisalimiana na mfuasi wa CCM

Uchaguzi wa mwaka 1995 ulikuwa wa kwanza wa vyama vingi tangu ule wa Tanganyika mwaka 1958 kwa Tnzania Bara na mwaka 1963 kwa Zanzibar, enzi za ukoloni wa Uingereza na mwarabu mtawalia, na wenye vyama vinne tu vichanga vya upinzani. Lakini mgombea wa wakati ule wa CCM Benjamin William Mkapa alikuwa na kibarua cha kutosha.

[ad_2]

Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *